- 119 viewsShambulizi la anga la Israeli katika shule inayoendeshwa na UN ambayo inazihifadhi familia katika kambi ya Nuseirat imewauwa watu 23 na kuwajeruhi wengine wengi, maafisa wa afya wa Palestina walisema Jumanne (Julai 16). Jeshi la Israeli lilisema katika taarifa yake limeshambulia kikundi cha “magaidi” ambao walikuwa wanafanya operesheni zao ndani ya shirika la Umoja wa Mataifa la Ujenzi na Misaada (UNRWA), baada ya kuchukua hatua za kuwaondoa raia waliokuwa hatarini katika eneo hilo. “Muda mfupi uliopita, kwa kutumia taarifa za kijasusi zilizo sahihi za Jeshi la Ardhini la Israeli na Shirika la Usalama la Israeli, Jeshi la Anga la Israeli IAF liliwashambulia magaidi waliokuwa wanafanya operesheni zao katika shule ya UNRWA katika eneo hilo la Nuseirat,” taarifa ilisema. Iliongeza kuwa IDF inafuatilia ripoti ya kuwa raia kadhaa walijeruhiwa kutokana na shambulizi hilo. Vita hiyo ilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji kutoka Palestina wa kikundi cha wanamgambo wa Hamas walipovamia mpakani na kushambulia jamii mbalimbali huko Israel, ikiuwa watu 1,200 na kuwateka watu 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israeli. Shambulizi la Israeli huko Gaza kulipiza kisasi lilianza siku hiyo hiyo kwa kushambulia kwa mabomu na limeendelea kwa miezi tisa pamoja na uvamizi wa ardhini ambapo mamlaka za afya Palestina zinasema imeuwa zaidi ya watu 38,000 na kujeruhi zaidi ya watu 80,000. Idadi kubwa ya waliojeruhiwa kutokana na vita hivyo imeongeza magonjwa kusambaa na utapiamlo kati ya wakazi asilimia 90 wa Gaza ambapo Umoja wa Mataifa unasema wamekoseshwa makazi, na kuweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya katika eneo hilo finyu. - Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #hospitali #nasserhospital
Shambulizi la Israel laua 23 na kujeruhi wengine katika shule ya UNRWA
- 27 Nov 2024 - The government has defended its ambitious livestock vaccination campaign aimed at combating viral diseases, despite opposition from some quarters.
- 27 Nov 2024 - Tanzania plans to honour its contracts with an Adani Group unit despite a U.S. indictment of its billionaire chairman Gautam Adani on accusations of bribery and fraud, a senior official at the ports authority said.
- 27 Nov 2024 - Angry residents of Kithogondo village in Ngurubani, Mwea, Kirinyaga County, blocked miraa vehicles from using the Mwea-Embu highway on Wednesday, following a tragic incident in which two children were killed by a speeding miraa truck on Tuesday.
- 27 Nov 2024 - The Orange Democratic Movement (ODM) grassroots elections have ignited a spirited contest for Nairobi's top leadership, pitting two seasoned politicians — Makadara MP George Aladwa and Westlands MP Tim Wanyonyi — against each other.
- 27 Nov 2024 - KMPDU has ordered intern doctors to down tools in protest following the death of one of their own, Dr. Francis Njuki, who reportedly took his own life due to frustration from his job.
- 27 Nov 2024 - Nearly 24 Kenyans have been arrested in connection with a case of online credit card fraud that led to losses worth over Ksh.1.1 billion.
- 27 Nov 2024 - The government has halted the recruitment process of job seekers abroad that was being conducted by the Ministry of Labour to fast-track the processing of the already selected applicants.
- 27 Nov 2024 - The government has halted the recruitment process of job seekers abroad that was being conducted by the Ministry of Labour to fast-track the processing of the already selected applicants.
- 27 Nov 2024 - A 40-year-old man who had been arrested for allegedly killing his wife in Kagio Town, Kirinyaga County has committed suicide at Kiamaciri Police Station in Mwea-West Sub-county.
- 27 Nov 2024 - The Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) has summoned four council members from Moi University to record a statement over the alleged embezzlement of Ksh2.2 billion through various infrastructural projects.