Shule na umma wanufaika Kilifi

  • | KBC Video
    8 views

    Shule katika kaunti ndogo ya Rabai kaunti ya Kilifi zinatarajiwa kunufaika na maji safi baada ya mbunge wa eneo hilo Anthony Kenga kufadhili uchimbaji wa visima vya maji kama njia moja ya kutatua tatizo la uhaba wa maji.Akizindua mradi wa uchimbaji kisima cha maji katika shule ya upili ya Canon Kuri, Kenga alisema kuwa uhaba wa maji katika eneo hilo umeathiri utoaji huduma hususan katika shule ambapo wasimamizi wa shule wanalazimika kununua maji kutoka sehemu za mbali na hivyo kutumia kiasi kukubwa cha fedha zilizotengewa shughuli za kimasomo. Aliahidi kuwa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi atazindua miradi zaidi ya maji katika shule ambayo pia itawafaidi wakazi wa vijiji vilivyo karibu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive