Wakazi wa wadi ya Mang’u, eneo la Gatundu Kaskazini, Kaunti ya Kiambu, walipigwa na butwaa baada ya sehemu ya kituo kipya cha elimu ya chekechea kubomolewa. Kituo hicho cha St. Francis ECDE, ambacho ni miongoni mwa zaidi ya vituo 300 vilivyojengwa na serikali ya kaunti ya Kiambu kiliharibiwa usiku huku baadhi ya milango ikivunjwa pamoja na vioo vya madirisha kupasuliwa — tukio ambalo wakazi wanasema huenda lilichochewa kisiasa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive