Sitikho young fc na Nakhwana Starlets ndio mabingwa wa mchuano wa DRM

  • | Citizen TV
    180 views

    Sitikho young fc na Nakhwana Starlets ndio mabingwa wa mchuano wa DRM upande wa wanaume na wanawake mtawalia.

    Kwenye fainali zilizopigwa katika uwanja wa shule ya msingi ya khalala kule webuye, sitikho walishinda kwa matuta manne kwa matatu dhidi ya milo fc. Kwa wasichana nakhwana waliibuka mabingwa kwa ushindi wa tatu moja dhidi ya mwangaza starlets. Washindi walituzwa fedha na vikombe.