Kwa sababu nimekuwa makini kila wakati ninapoandaa taarifa, kila wakati ninaposikiliza kauli fulani, hasa kauli za kisiasa, lazima nichunguze ukweli. Lazima nithibitishe mara mbili ili kuwa na uhakika. Kukosekana kwa mafunzo kama hayo, unafahamu kwamba wakati mwingine unatumia fursa inapokuja.
Hata hivyo Chitete anasema baadhi ya mashirika na idara za serikali bado zinasita kutoa taarifa zinazohitajika kuthibitisha habari hizo, na hatua hii ya kuzuia taarifa inatatiza juhudi zao za uandishi.
Suzgo Chitete, Mwandishi wa Habari gazeti la The Nation anaeleza:Kwa mfano, nina masuala na Wizara ya Mambo ya Nje, kwa sababu nilitaka habari kuhusu sifa kwa wanadiplomasia wote walioteuliwa tangu 2020. Suala ni kuona kama kweli wale walioteuliwa wana hadhi ya kutosha kuitumikia Malawi. Serikali imekuwa ikisema. Tunaajiri watu sahihi. Lakini tuna wasiwasi wakati mwingine kwamba hao sio watu sahihi, lakini kisiasa hawa ni watu sahihi.
Tume ya Haki za Binadamu
Katika uamuzi wake, Tume ya Haki za Binadamu ya Malawi, iliyopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria ya upatikanaji wa habari, iliikosoa Wizara ya Mambo ya Nje kwa kukataa kutoa taarifa za umma zilizoombwa na Chitete.
MISA na UNDP
Matonga anasema mbali na mafunzo hayo, MISA Malawi na UNDP pia wanaufanyia kazi mradi mpya ambao utasaidia kuhamasisha taarifa za kuaminika za habari wakati wa uchaguzi mkuu 2025.
Golden Matonga, Mwenyekiti wa MISA Malawi anaeleza: "MISA, kwa upande wetu, tutazindua mradi kamili wa kuangalia taarifa zilizo za kweli kwa msaada kutoka UNDP. Mradi unaitwa “I verify” ambapo tutaweza kuuliza umma kwa ujumla kuripoti kwenye tovuti, kesi za taarifa potofu na zisizo sahihi, na tutakuwa na timu ya wataalam ambao watakwenda na kuondoa taarifa hizo bandia na kushirikisha taarifa sahihi."
Matonga anaamini juhudi hizi zitawapa waandishi wa habari ujuzi na vifaa vinavyoweza kupatikana kwa urahisi ili kuangalia taarifa za ukweli katika uandikaji wa ripoti zao na kuwawezesha wananchi kufahamu wenyewe, ni Habari zipi zenye uhakika na za kuaminika.
Imetayarishwa na Mwandishi Lameck Masina kutoka Lilongwe, Malawi.
#habaripotofu #malawi #lilongwe #waandishi #habari #MISA #kusinimwaafrika #usahihi #uaminifu #voa #voaswahili #mafunzo #MISA