Tahadhari ya Mafuriko

  • | Citizen TV
    1,647 views

    Huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha sehemu kadhaa nchini, wakaazi wa kaunti za Garissa na Tana River wameonywa kuhusu uhaba wa maji safi kufuatia kuchafuka na njia za kusambaza maji. Kampuni ya maji ya Garissa ya GAWASCO sasa ikiwataka wakaazi kujipanga licha ya mvua kuendelea kushuhudiwa. Aidha, tahadhari imetolewa kwa wakaazi wa eneo la kati kuhamia maeneo salama kufuatia mvua inayonyesha.