TikTok yanufaika na matangazo mubashara ya ngono inayohusisha watoto

  • | BBC Swahili
    437 views
    Kutokana na uwepo wa video nyingi za kuburudisha na vichekesho kadha wa kadha, haishangazi kuona kwamba TikTok inapendwa na vijana nchini Kenya. Pia ni njia moja wapo ya wao kujipatia pesa kupitia kipengele cha kurusha mubashara na kupata zawadi mbalimbali. Lakini kuna upande mbaya zaidi, ambapo wasichana wadogo wenye umri wa miaka 15 - wanauza maudhui ya ngono wanapokuwa mubashara, huku wengine wakiajiriwa na ‘madalali wa kidijitali'. BBC Africa Eye inachunguza unyanyasaji wa kijinsia kwa wasichana na ni nani anafaidika? #bbcswahili #AfrikaEye #bbcafrikaeye Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw