Skip to main content
Skip to main content

Tim Wanyonyi ashabikiwa kwa kuwakilisha walemavu

  • | Citizen TV
    125 views
    Duration: 1:26
    Kutangaza rasmi kwa Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi kwenye kinyang'anyiro cha ugavana wa kaunti ya Bungoma mwaka wa 2027 , sio tu kwa manufaa yake mwenyewe ila ni mfano wa kuigwa kwa baadhi ya walemavu . Henry Opilo Mkazi wa Musikoma kwenye Eneo bunge la Kanduyi anasema kuwa walemavu hawajakuwa wakijihusisha kwenye siasa moja kwa moja ,ila sasa kando na kutunukiwa aslimia tano kuwakilishwa wana nafasi ya kumenyana na watu wengine. Opilo anasema kuwa Wanyonyi ni ishara ya siasa ya amani na ujio wake utapunguza vurugu ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika kaunti ya Bungoma. Kwa zaidi ya miaka kumi baada ya ujio wa Ugatuzi nchini, Opilo anasema kuwa bado kuna mengie ambayo yanafaa kutekelezwa ili kuafiki malengo ya ruwaza ya 2030.