'Tulimfunua na kuona amekuwa wa bluu'

  • | BBC Swahili
    738 views
    Idadi ya watoto wanaofariki kwa baridi kali Gaza inazidi kuongezeka. Hali ya hewa ya baridi huko Gaza inagharimu maisha ya watoto wachanga ambapo sasa idadi ya waliofariki imefikia sita ndani ya wiki moja huku mashambulizi ya Israel yakiendelea. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na mtoto wa wiki tatu Sila na mtoto wa mwezi mmoja Ali al-Batran ambaye alifariki akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya yeye na pacha wake kukimbizwa hospitalini. #bbcswahili #gaza #israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw