Ugavi wa ardhi ya Kisaju Trust wazua utata

  • | Citizen TV
    520 views

    Jamii ya Kaputie kutoka kaunti ya Kajiado imetofautiana vikali na mapendekezo ya serikali ya kaunti ya Kajiado kugawa kipande chao cha ardhi cha Kisaju trust Kilichoko Isinya. Wanasema kati ya Ekari 1757.67, ni ekari 300 pekee zimetengewa jamii wakisema hatua hiyo iliafikiwa bila kuwahusisha wanachama ambao wanapaswa kumiliki kipande hicho cha ardhi chenye dhamani ya zaidi ya shilingi Billioni 35.