Kesi ambapo jaji mkuu Martha Koome anapinga mamlaka ya tume ya huduma za mahakama kwenye masuala ya uteuzi katika idara ya mahakama, na usimamizi wa masuala ya ndani ya idara hiyo, ilikosa kuendelea hivi leo. Hii ni baada ya wakili Nelson Havi aliyewakilisha mlalamishi, kudadisi uhalali wa jopo la majaji watatu linaloongozwa na jaji Charles Kariuki ambalo lilitarajiwa kusikiza kesi hiyo. Kupitia wasilisho lake, Havi alidai upo mkinzano wa maslahi katika uteuzi wa majaji hao na jaji mkuu ambaye ndiye mlalamishi katika kesi hiyo. Kando na hayo, alitaka majaji wawili kujiondoa kutoka kwenye jopo hilo. Mengi zaidi ni kwenye kitengo cha mizani ya haki.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive