Uhalifu isiolo : Shambulizi dhidi ya MCA lalaaniwa

  • | KBC Video
    23 views

    Wawakillishi wadi wa kaunti ya Isiolo wameshutumu kisa ambapo mwakilishi wa wadi ya Burat Nicholas Lorot, anadaiwa kushambuliwa siku ya Jumatano mjini Isiolo. wakiongozwa na spika wa bunge la kaunti hiyo Mohamed Roba Qoto, wawakilishi wadi hao walielezea kutoridhishwa na kisa hicho wakisema kinaashiri kudorora kwa usalama katika eneo hilo. Roba alisema utekelezaji kikamilifu wa sheria utaweza kuwafichua watekelezaji wa uhalifu huo na kiini chake. Wakazi wa Isiolo wamehimizwa kujiepusha kueneza uvumi kuhusu kisa hicho na kuwapasha habari maafisa wa usalama iwapo wana taarifa itakayofanikisha kukamatwa kwa wahusika .

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News