- 737 viewsDuration: 3:16Ukosefu wa fedha za kufanikisha utafiti kwenye vyuo vikuu mbali mbali nchini umetajwa kama changamoto kubwa inayolemaza juhudi za waatalam kuendeleza utafiti kuhusu masuala mbali mbali. Wakizungumza huko Kajiado watalamu wanasema licha ya uwezo wao na ujuzi wa kuendeleza utafiti ambao unalenga kuleta suluhu ya changamoto mbali mbali, ufadhili wa kuwezesha utafiti huo ndio kikwazo kikubwa.