Ulinzi mkali waimarishwa karibu na bunge na Ikulu ya Nairobi

  • | BBC Swahili
    3,249 views
    Waandamanaji wamejitokeza barabarani kote nchini Kenya hii leo huku hasira ikiongezeka kuhusu mapendekezo ya muswada wa sheria ya fedha 2024 ya serikali kuongezwa ushuru. - Kuna ulinzi mkali karibu na bunge na Ikulu ya Nairobi, ambapo maandamano makubwa zaidi yanatarajiwa kufanyika. - Maandamano hayo yameongozwa na kizazi cha vijana cha 'Gen Z' nchini Kenya, wakimtaka Rais William Ruto aondoe kodi wanayoona kama adhabu. - Watu wawili walifariki katika maandamano sawa na haya wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na mtu mmoja anayeaminika kupigwa risasi na polisi. #bbcswahili #kenya #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw