UMILIKI WA ARDHI TAITA TAVETA

  • | Citizen TV
    152 views

    Wakazi wapatao 1,055 huko Mwatate na Kaloleni kaunti ya Taita Taveta wamepata hati miliki za ploti zao hii ikiwa mwamko mkubwa kwa wenyeji ambao wamekua wakiishi kwa woga wa kufurushwa.

    Akizungumza baada ya kukagua zoezi linaloendelea la kuweka alama za ardhi eneo la Kaloleni, Gavana wa Taita Taveta Andrew Mwadime , ameeleza kuwa ndio mwanzo tu wa kuhakikisha kuwa changamoto za ardhi zilizoko kaunti hiyo zinazikwa katika kaburi la sahau.