Umoja wa Mataifa waidhinisha operesheni mpya ya kijeshi nchini

  • | Citizen TV
    536 views

    Baraza la umoja wa mataifa kuhusu usalama limeidhinisha operesheni mpya ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika kudhibiti usalama nchini Somalia kuanzia Januari mwaka ujao. Wanachama14 kati ya 15 wa baraza hilo waliidhinisha operesheni hiyo ambapo wahudumu 12,626 watakuwa chini ya kikosi cha udhibiti na msaada (AUSSOM). Hii ni baada ya Kikosi cha awali kukamilisha majukumu yake. Kikosi cha AUSSOM kitaendelea kukabiliana na magaidi wa kundi la Al-Shabaab na kuwalinda raia wa Somalia. Marekani ilijiondoa kwenye uamuzi huo.