Urusi yaonya dhidi ya “propaganda” za ajali ya ndege ya Azerbaijan

  • | BBC Swahili
    545 views
    “Itakuwa makosa kueneza propaganda kabla ya uchunguzi. Hatutafanya hivyo, na hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo. Tunahitaji kusubiri uchunguzi ukamilike.” Urusi yaonya dhidi ya “propaganda” zinazoenezwa kuhusu ajali ya ndege ya Azerbaijan iliyotokea siku ya krismasi na kuua watu 38 nchini Kazakhstan. Baada ya picha na video ya mabaki ya ndege hiyo kusambaa mitandaoni baadhi ya wataalamu wa anga walisema kuwa ndege hiyo ya Azerbaijan Airlines huenda ilipigwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya juu ya jimbo la Chechnya nchini Urusi na vyombo vya habari vya serikali vya Azerbaijan vilinukuu maafisa wakisema kombora la Urusi lilihusika. #bbcswahili #urusi #kazakhstan Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw