Vijana wa Nyamira wakosoa serikali kuhusu utekaji nyara

  • | Citizen TV
    953 views

    Wakazi wa matabaka mbalimbali wakiwemo vijana, viongozi na mawakili kutoka kaunti ya Nyamira wamejiunga na wenzao kote nchini kukemea utekaji nyara wa vijana unaoendelea nchini. Wakizungumza kwenye mkutano wa vijana kutoka Nyamira uwanjani Nyamaiya eneo bunge la Mugirango Magharibi, vijana hao wameitaka serikali kuwapeleka kortini wenye hatia badala ya kuwapeleka kusikojulikana. Hali kadhalika, Vijana hao wamelalamikia ukosefu wa maendeleo katika kaunti hiyo, hali wanayodai inachangiwa na utepetevu wa viongozi waliochaguliwa.