Vijana wa Wote kaunti ya Makueni wasitisha shughuli za ujenzi wa nyumba za bei nafuu

  • | Citizen TV
    162 views

    Shughuli za ujenzi katika mradi wa nyumba za bei nafuu mjini Wote kaunti ya Makueni zimetatizika baada ya vijana wasio na kazi kufika kwenye mradi huo na kuusitisha wakilalamikia kutopewa nafasi za ajira kwenye mradi huo. Kulingana nao, rais Wiliam Ruto aliahidi kuwa miradi hiyo itakuwa ikiwafaa wakazi wa maeneo inakojengwa. Aidha, baadhi wanalalamika kuwa vijana kutoka maeneo mengine ya mbali wamepewa ajira. kadhalika wanalalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi kwa wale wachache waliopewa kibarua.