Vijana waanzisha kampeni dhidi ya mihadarati Trans Nzoia

  • | Citizen TV
    494 views

    Kundi moja la vijana katika Kaunti ya Trans Nzoia limeanzisha harakati za kuwahamasisha vijana wenzao kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na badala yake kujihusisha na shughuli zinazowaletea manufaa. Wakizungumza katika eneo la Kiminini baada ya kuandaa mashindano ya soka katika eneo hilo, vijana hao walisema wameanzisha kampeni hiyo kufuatia ongezeko la visa vya vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa za kulevya katika jamii yao. Walisema kupitia michezo, vijana wanaweza kupata riziki na kuepuka visa vya uhalifu.