- 1,696 viewsDuration: 3:21Vijana waliopokea mafunzo kupitia shirika la NYS watapewa kipaumbele katika shughuli ijayo ya usajili wa makonstebo wa polisi. Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, amesema kuwa vijana hao watatakiwa kujitokeza katika vituo vya usajili kwenye kaunti ndogo wanakotoka au katika kituo mbadala kilicho kwenye makao makuu ya shirika la NYS, katika eneo la Ruaraka, kaunti ya Nairobi. Huduma hiyo ya polisi pia imetangaza mabadiliko muhimu katika orodha ya vituo vya usajili vya kitaifa ambapo shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 17 mwezi huu. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive