Viongozi Kajiado waitaka serikali kukomesha utekaji nyara

  • | Citizen TV
    1,247 views

    Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali kukumoesha visa vya utekaji nyara kwa vijana ambavyo vimeonekana kuongezeka . Mbunge wa Kajiado Kaskasini Onesmus Ngogoyo na seneta wa Kajiado Samuel Kanar Seki wanasema licha ya jamaa ndugu na marafiki ya waliotekwa nyara kutaka majibu kuhusu waliko wapendwa wao , hadi sasa serikali haijatoa imesalia kimya kuhusu waliko vijana hao. sasa wanataka jamii za kimatiafa kupitia mabalozi wao humu nchini kujitokeza na kukemea visa hivyo vya utekaji nyara.