Viongozi na wakazi wa Kilifi wataka mateka waachiliwe

  • | Citizen TV
    772 views

    Viongozi kutoka kaunti ya kilifi pamoja na wakazi wa kaunti hiyo wamelaani visa vya utekaji nyara vinavyoendelea humu nchini. Seneta wa kaunti hiyo stewart madzayo akizungumza na wanahabari mjini malindi amemshauri rais William ruto kukomesha utekaji nyara huo. Aidha Madzayo ameahidi kuongoza maandamano endapo waathiriwa wa utekaji nyara hawataachiliwa huru.