Viongozi wa dini wataka utulivu nchini

  • | Citizen TV
    326 views

    Viongozi wa kidini wametoa wito kwa wananchi kudumisha amani hasa wakati huu ambapo kwa mara ya kwanza taifa linashuhudia mchakato wa kumwondoa afisini naibu wa Rais Rigathi Gachagua. Wakizungumza eneo la chesikaki eneobunge la mlima elgon, viongozi hao wamesema kuwa viongozi wa kisiasa wangetumia muda wao kushughulikia maswala ya maendeleo na wala sio swala nzima la kumwondoa mamlakani naibu rais. Wamewataka wananchi kuwa watulivu wakati wa zoezi hilo.