- 4,930 viewsDuration: 2:49Mwenyekiti wa Tume ya haki na Amani ya baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Tanzania Yuda Tadei Ruwaichi amekashifu ghasia za uchaguzi zilizoshuhudiwa nchini Tanzania. Akiongoza misa kwa waathiriwa wa ghasia hizo, Askofu huyu Mkuu wa Jimbo la Dar Es Salaam, amelaumu serikali kwa kutumia nguvu akisema adhabu kwa waandamanaji si Kifo. Rais wa zamani wa Botswana Ian Khama amekosoa uchaguzi huo akisema hatambui uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.