Viongozi wa SADC na EAC wajadili usalama katika eneo la DRC

  • | VOA Swahili
    422 views
    Kikao kinachowakutanisha pamoja wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kimefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mkutano huo umejadili hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amehudhuria kikao hicho, huku Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, alishiriki kwa njia ya mtandao. Kikao hicho kinaongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Kenya, William Ruto. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pia alikuwepo katika kikao hicho cha dharura kujadili hali ya mashariki mwa DRC. Viongozi wengine waiohudhuria mkutano huo ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema. Ripoti ya mwandishi wa VOA, Amri Ramadhani Picha zote na Idara ya Habari: MAELEZO #voaswahili #afrika #congo #drc #goma #m23 ⁣#sadc #eac #mawaziri #mamboyanje #marais