Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa upinzani wamshutumu Rais Ruto kwa kuzorotesha sekta muhimu na kuongeza gharama ya maisha

  • | Citizen TV
    3,267 views
    Duration: 1:26
    Viongozi wa upinzani wamemshutumu Rais William Ruto kwa kile wanachodai ni kuharibu sekta muhimu za taifa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake. Wanasema elimu, afya na biashara zimezorota, huku wananchi wakikabiliwa na gharama ya juu ya maisha. Viongozi hawa wakijumuisha aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka walikuwa wakizungumza katika hafla tofauti maeneo ya Kayole hapa Nairobi, Limuru na Makueni