Viongozi wakanusha madai ya mashauriano

  • | KBC Video
    20 views

    kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa, kimani Ichung’wah, amejikuta tena akikosolewa na baadhi ya viongozi wa kaunti ya kiambu kufuatia kauli zake za hivi karibuni. Ichung’wah alidai kuwa wabunge kutoka kiambu walishauriwa wakati wa mchakato wa kuteua waziri mpya wa kaunti hiyo.Wa kwanza kumkosoa alikuwa seneta wa kiambu, karungo thang’wa, ambaye alitumia mitandao ya kijamii kukanusha madai hayo. Thang’wa aliongeza kuwa madai ya ichung’wah yalipotosha, na akaeleza kuwa hata kama angepewa nafasi, asingempendekeza waziri wa kilimo wa sasa kwani hamfahamu vyema. Viongozi wengine waliunga mkono ukosoaji huo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive