Viongozi wakuu duniani wahudhuria mazishi ya papa francis

  • | Citizen TV
    4,897 views

    Maelfu ya waombolezaji walikongamana jijini Roma Italia kumuaga Papa Francis katika misa takatifu ya mazishi iliyofanyika katika kanisa katoliki la St. Peters Basilica jijini Vatican. Kadinali Giovanni Battista Re, aliyeongoza misa hiyo ya mazishi, alimsifu Papa Francis kutokana na juhudi zake za kuleta umoja, msamaha na kufungua milango ya kanisa kwa watu wote bila ubaguzi.