Vita vya kibiashara vyatokota kati ya Marekani na China. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    13,605 views
    China imeongeza zaidi ushuru wake kwa bidhaa za Marekani hadi asilimia 125 na kuzidisha vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ya uchumi mkubwa duniani. Hatua hiyo ni ya kujibu ongezeko la ushuru wa Marekani kwa bidhaa za China hadi asilimia 145. Wakati huohuo, dhahabu imepanda bei katika masoko huku waekezaji wakiiona kama bidhaa salama kwa biashara.