Waandamanaji wajitokeza eneo la Aga Khan Walk kushinikiza waliotekwa nyara waachiliwe

  • | Citizen TV
    78,830 views

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu , vijana pamoja na walioachiliwa baada ya kutekwa nyara, wameandaa maandamano Jumatatu hii ambayo walisema yatafanyika mitaani kote nchini na kwenye mitandao ya kijamii. Maandamano hayo yakilenga kuishinikiza serikali kuwaachilia waliotekwa nyara na kukomesha hulka hiyo ya kukiuka katiba. Wanahabari wetu wako maeneo tofauti kutathmini hali, na sasa tunaungana nao mubashara watufahamishe yanayojiri katika maeneo walipo.