Waandishi na wataalamu Cameroon wajiandaa kudhibiti taarifa potofu kuleta machafuko

  • | VOA Swahili
    28 views
    Raia wa Cameroon watapiga kura mwaka ujao kumchagua rais kwa muhula mwingine wa miaka saba. Chaguzi za awali katika taifa hili la Afrika ya Kati zilikumbwa na taarifa potofu ambazo zilichochea machafuko kwenye mitandao ya kijamii. Sasa, waandishi wa habari na wataalamu wa vyombo vya habari wanasema wanachukua hatua za mapema ili kuzuia kurudiwa kwa masuala haya. Amboh Vanessalizzy, mtayarishaji wa Maudhui huko Buea, alikuwa akipitia mitandao ya kijamii wakati habari zilipoibuka kuwa rais wa Cameroon, Paul Biya, amefariki. Bila njia yoyote ya uthibitisho, alisubiri mawasiliano rasmi hadi serikali ilipotoa taarifa ya kukanusha uvumi wa kifo cha Rais kama ndoto tu Amboh Vanessalizzy, Mtengenezaji Maudhui asema:Kwa kadiri tunavyotaka mabadiliko, simuombei kifo mtu yeyote. Taarifa potofu kama zile zinazomhusu rais zinaweza kuwa za mara kwa mara, hasa wakati wananchi wa Cameroon wakielekea kwenye uchaguzi mwaka ujao. Batata Boris-Kaloff]], Meneja wa Kituo cha CBS Buea aeleza: "Tayari ninajitayarisha kukabiliana na taarifa potofu za uchaguzi ambazo zinaweza kuja. Uwe na uhakika, huko Buea, kuna wanasiasa na kutakuwa na mijadala kuhusu miradi hapa na pale." #cameroon #waandishi #habaripotofu #chaguzi #ghasia #voaswahili - - - - - VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi. Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu. Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000. Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru. Jiunge na VOA Swahili: » Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc »Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI »Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus »Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI »Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/ »Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili »Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili »Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili »Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili