Waandishi wa habari Msumbiji wanavyopambana taarifa za uongo

  • | VOA Swahili
    16 views
    Msumbiji ambako kuenea taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kunawalazimu waandishi wa habari nchini humo kuwa mstari wa mbele katika kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo . ⁣ Hapa katika chumba cha habari cha Evidencias, mjini Maputo, Msumbiji, Reginaldo Tchambule na timu yake wanafanya kazi ya kuweka rekodi sawa katika jitihada za kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. ⁣ ⁣ Yeye na mwenzake Nelson Mucandze, wanasema walianzisha pamoja gazeti na lile la mtandaoni miaka minne iliyopita kwa sababu mashirika mengine mengi hayakuwa yakikagua ukweli au kutumia taarifa na uchambuzi katika kuripoti kwao. Tchambule anasema hadhira yao ilianza kufuatilia kwa haraka.⁣ Reginaldo Tchambule, Evidencias Editor anaeleza: “Gazeti la Evidencias linaweza kuwa limepata muonekano na umaarufu mkubwa katika muda mfupi, kwa sababu ya jinsi tulivyozingatia uandishi wa habari wenyewe. Wakati fulani tulikuwa na ukurasa ambapo tulichunguza habari kuu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.” ⁣ ⁣ Mwaka huu, Tchambule aliripoti kwa nini Ossufo Momade, kiongozi wa Renamo, chama kikuu cha upinzani cha Msumbiji, hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa wakati wa kampeni za urais. ⁣ Evidencias ilianza kuchunguza picha kwenye mtandao wa Facebook wa mgombea ambapo ilionekana Momade alikuwa akifanya kazi nje ya nchi. ⁣ ⁣ Ripoti ya Amarilis Gule VOA Maputo.⁣ ⁣ #habaripotofu #msumbiji #maputo #chumbachahabari #Evidencias #gazeti #reginaldotchambule #voa #voaswahili - - - - - VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi. Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu. Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000. Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru. Jiunge na VOA Swahili: » Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc »Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI »Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus »Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI »Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/ »Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili »Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili »Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili »Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili