Katika mji wa Goma, kundi la waandishi wa habari wa Congo wanakabiliana na habari potofu chungu nzima kuhusu afya na matibabu, ambazo ni hatari kubwa sana kwa umma.
Katika eneo linalopambana na changamoto za afya na kukumbwa na vita, waandishi wa kubaini habari za uongo katika jarida la Eleza ukweli, wanatafuta habari za ukweli kuhusu fikra zinazoambatana na ugonjwa mpox ambao awali ulikuwa unajulikana kama ugonjwa kutoka kwa nyani. Habari za uongo zinasema kwamba ugonjwa huo haupo kabisa na kwamba yanayosemwa ni upele tu ambao hauna madhara.
Aline Kataliko anasema kazi yao ni muhimu sana kwa afya ya umma na katika kujenga imani katika jamii.
Aline Kataliko wa Eleza Fact: 'Kuna uvumi kuhusu mpox, unaosema kwamba lengo la chanjo ni kuondoa kizazi cha raia wa Congo. Tunaangazia hatari za uvumi huo na namna unavyoweza kuathiri jamii yote kwa jumla na kuzuia juhudi za kumaliza maambukizi."
Habari Potofu
Tangu mwaka 2021, waandishi wa habari 25 katika jarida la Eleza ukweli, akiwemo Joel Alimasi Kitambala, wamekuwa wakiangazia na kueneza habari kuhusu hatari za habari potofu. Joel Alimasi Kitambala ni mwandishi wa habari katika Eleza Ukweli.
Joel Alimasi Kitambala wa Eleza Fact: Kutambua ukweli, tunatumia maneno muhimu na kila wakati kuna chapisho ambalo lina maneno hayo, tunapata taarifa kuhusu chapisho hilo. Kama kuna hja ya kuchambua jarida hilo, waandishi wa kutafuta ukweli wanapewa jukumu wanaolifanyia kazi.
Makala yanayochapishwa na Eleza ukweli, yanachapishwa kwenye wavuti, na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kutangazwa kwenye vituo vya radio ili kuwafikia wale wasiotumia internet.
Taarifa za Uongo juu ya Afya na Tiba
Kuna taarifa nyingi za uongo kuhusu afya na tiba kama taarifa zilizotolewa kuhusu mpox. Mwandishi wa habari Joylen Kazimoto aliripoti kuhusu habari potofu kuhusu virusi vya Corona kwa kutumia njia ya internet - podcast. Joylen Kazimoto ni mwandishi wa Eleza ukweli.
Mwandishi wa habari Zanem Nety Zaidi ameandaa ripoti ifuatayo kutoka Goma, DRC. Inasomwa na Kennes Bwire.
#habaripotofu #drc #goma #waandishi #voa #voaswahili
- - - - -
VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi.
Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.
Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000.
Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru.
#habaripotofu #drc #goma #waandishi #voa #voaswahili
Jiunge na VOA Swahili:
» Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc
»Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI
»Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus
»Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI
»Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/
»Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili
»Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili
»Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili
»Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili