Waandishi wanamatumaini ya kukabiliana na habari potofu

  • | VOA Swahili
    74 views
    Raia wa Cameroon watapiga kura mwaka ujao kumchagua rais kwa muhula mwingine wa miaka saba. Chaguzi za awali katika taifa hili la Afrika ya Kati zilikumbwa na taarifa potofu ambazo zilichochea machafuko kwenye mitandao ya kijamii. Sasa, waandishi wa habari na wataalamu wa vyombo vya habari wanasema wanachukua hatua za mapema ili kuzuia kurudiwa kwa masuala haya. Amboh Vanessalizzy, mtayarishaji wa Maudhui huko Buea, alikuwa akipitia mitandao ya kijamii wakati habari zilipoibuka kuwa rais wa Cameroon, Paul Biya, amefariki. Bila njia yoyote ya uthibitisho, alisubiri mawasiliano rasmi hadi serikali ilipotoa taarifa ya kukanusha uvumi wa kifo cha Rais kama ndoto tu Amboh Vanessalizzy, Mtengenezaji Maudhui asema:Kwa kadiri tunavyotaka mabadiliko, simuombei kifo mtu yeyote. Taarifa potofu kama zile zinazomhusu rais zinaweza kuwa za mara kwa mara, hasa wakati wananchi wa Cameroon wakielekea kwenye uchaguzi mwaka ujao. Batata Boris-Kaloff]], Meneja wa Kituo cha CBS Buea aeleza: "Tayari ninajitayarisha kukabiliana na taarifa potofu za uchaguzi ambazo zinaweza kuja. Uwe na uhakika, huko Buea, kuna wanasiasa na kutakuwa na mijadala kuhusu miradi hapa na pale." Ripoti ya Njodzeka Danhatu wa VOA. #cameroon #waandishi #habaripotofu #chaguzi #ghasia #voaswahili