- 45 viewsKatika wiki za hivi karibuni, kikundi cha M23 kimerudi tena kwenye vichwa vya habari vya kimataifa kwa kuiteka Goma, mji muhimu upande mashariki mwa Congo. Lakini hawa ni nani (M23), na kwa nini kuibuka kwao upya kumechochea upinzani, ghasia na wasiwasi wa kimataifa? Haya ndiyo unapaswa kuyafahamu kuhusu M23, chimbuko lao, na mgogoro unaosambaa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kikundi cha waasi wa M23, au Harakati za Machi 23, zimepewa jina hilo kutokana na mkataba wa amani wa 2009 kati ya serikali ya Congo na kikundi cha waasi kinacho ongozwa na Watutsi, CNDP. Makubaliano hayo yaliahidi kuwaingiza waasi katika jeshi la taifa na ulinzi kwa jamii za Watutsi lakini halikutekelezwa kikamilifu, na kuzusha uasi wa M23 mwaka 2012. Licha ya kushindwa mwaka 2013, kikundi hicho kilirejea tena mwaka 2021, na kuchochea mgogoro huko mashariki mwa Congo. Wiki hii, M23 ilichukua udhibiti wa Goma, mji wenye watu takriban milioni 2 na kituo cha kibinadamu, ukiwemo uwanja wake wa ndege, na kukata njia muhimu za kufikisha misaada. Shambulizi hilo liliuwa watu kadhaa walioachwa mitaani, hospitali zilielemewa, na taarifa za uporaji na uvunjifu wa haki za binadamu. Maelfu wameukimbia mji huo, wakati waandamanaji mjini Kinshasa walishambulia balozi kadhaa za nchi ambazo zinazishutumu kuwa zinaisaidia M23, ikiwemo Rwanda. DRC inaishutumu Rwanda kwa kuisaidia M23 ili kunyakua utajiri wa madini yaliyoko katika kanda hiyo – madai ambayo yanakanushwa na Rwanda, licha ya ripoti za Umoja wa Mataifa kuunga mkono tuhuma za Congo. Mgogoro huo unaakisi vita kadhaa vya Congo huko nyuma, ambavyo viliuwa mamilioni na kuuyumbisha ukanda huo. Huku mivutano ikiongezeka, jumuiya ya kimataifa inahofia mgogoro huo unaweza kuongezeka kuwa vita vipana zaidi vya kanda hiyo, kuzidisha hali mbaya zaidi ya maafa ya kibinadamu na kutishia amani iliyo hatarini katika eneo la Maziwa Makuu. - VOA #voaswahili #afrika #rwanda #drc #m23 #dacs
Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa Congo ni nani?
- 4 Feb 2025 - President William Ruto has pledged to bring back the five chiefs who were abducted by suspected Al-Shabaab militia on Monday in Mandera County, saying the country will not cede an inch to criminals.
- 4 Feb 2025 - A 7-year-old girl has died after being poisoned by her father, who reportedly mixed petrol with an unknown chemical following an alleged disagreement with his ex-wife, in Minyere village, in Ndhiwa, Homabay County.
- 4 Feb 2025 - Uganda has deployed more than 1,000 extra soldiers into east Congo in the last week near an area where the Kinshasa government is fighting M23 rebels, four diplomatic and U.N. sources said, heightening fears of a regional escalation.
- 4 Feb 2025 - A suspected chicken thief has been lynched at Diambo Estate in Ngurubani town in Mwea-East sub-county, Kirinyaga County.
- 4 Feb 2025 - The amount to serve as upkeep for first and second year students during the 2024/25 Academic Year
- 4 Feb 2025 - Carlo Ancelotti said Kylian Mbappe would miss Real Madrid’s upcoming Copa del Rey quarter-final against Leganes with a bruised calf and backed his club’s complaints about Spanish refereeing on Tuesday. French striker Mbappe was hacked down by Espanyol’s…
- 4 Feb 2025 - Spain coach Luis de la Fuente on Tuesday told the forced kiss trial of ex-football federation chief Luis Rubiales that he initially knew nothing of the scandal's scale or efforts to silence it. Rubiales provoked worldwide outrage for the kiss on Jenni…
- 4 Feb 2025 - KMPDU says the strike will take effect from midnight
- 4 Feb 2025 - AC Milan secured a loan deal for Chelsea forward Joao Felix as the Serie A club made four late signings in the winter transfer window in a bid to revive their season. In a statement Milan said that Portugal forward Felix, who only scored one league goal…
- 4 Feb 2025 - The plan had previously been suspended after Kenyans raised concerns.