Wademokrat wajibu hotuba ya Trump, wahofia mabadiliko yenye 'vurugu'

  • | VOA Swahili
    653 views
    Wademokrat wametahadharisha kupanda kwa bei na mabadiliko yenye “vurugu" kufuatia hotuba ya Rais Donald Trump Bungeni siku ya Jumanne (Machi 4). Seneta Elissa Slotkin alizungumza kwa upande wa Chama cha Demokratiki kujibu hotuba ya Rais Trump, akitoa wito ipatikane suluhu katika “mfumo wa uhamiaji uliovunjika” Marekani na kumshutumu Trump kwa “kujiegemeza kwa madikteta”. Slotkin aliwasihi raia wa Marekani “wasijiengue” na waendelee kufuatilia masuala ya siasa. - Reuters #POTUSAddress, #trump #congress #voa #democrats #seneta #elissaslotkin