Wafungwa wanawake walivyobakwa Goma, DRC

  • | BBC Swahili
    9,880 views
    Manusura wa moto mkali ulioteketeza jela moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuwachoma hadi kufa wanawake 132 na watoto 26, wameiambia BBC kuwa wanapigania haki yao, ila hawana imani ya kuipata. Inadaiwa kuwa moto huo ulianzishwa na wafungwa wanaume waliojaribu kutoroka jela hiyo ya mashariki ya mji wa Goma mwezi uliopita wakati kundi la m23 liliendelea kuuvamia ukanda huo. Zaidi ya watu elfu 4 wanadaiwa kutoroka gerezani lakini ni wanawake wachache tu waliofanikiwa kutoroka. Wengi wao walibakwa na wafungwa wa kiume, kulingana na manusura.