Wahudumu wa bodaboda kaunmti ya Kwale watakiwa kutojihusisha na uhalifu

  • | Citizen TV
    132 views

    Wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Kwale wametakiwa kutojihusisha na visa vya uhalifu na kuripoti kwa maafisa wa polisi washukiwa wa uhalifu miongoni mwao. Mwenyekiti wa muungano wa bodaboda nchini (BAK) Kevin Mubadi amewataka wanabodaboda kushirikiana na vitengo vya usalama kwa kutoa taarifa kuhusu vijana wanaotumia pikipiki kuhangaisha wenyeji kwa mapanga. Akizungumza wakati wa uchaguzi wa muungano huo ambapo Mahmoud Rajab amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Kwale, Mubadi amesema wataendelea kuleta mabadiliko ya kufaa sekta ya bodaboda nchini.