Wakaazi wa New Jersey washuhudia droni zisizojulikana

  • | VOA Swahili
    87 views
    Idadi kubwa ya droni zisizotambuliwa zimeripotiwa kuruka katika maeneo ya New Jersey na East Coast katika wiki za karibuni, ikizua wasiwasi na dhana juu ya nani na kwa nini zinatumwa huko. Darzeni ya walioshuhudia wameripoti kuziona droni hizo huko New Jersey tangu mwezi Novemba. Hapo awali, droni hizo zilionekana zikiruka katika upeo wa Mto Raritan, mkondo wa maji unaoelekea katika hifadhi ya maji ya Round Valley, ni mwamba unaohifadhi maji ya jimbo hilo, umbali wa kiasi cha kilometa 80 magharibi mwa Jiji la New York. Lakini mara droni hizo ziliripotiwa kuonekana katika jimbo lote, ikiwemo karibu na Picatinny Arsenal, kituo cha jeshi la Marekani cha utafiti na utengenezaji, na juu ya eneo la uwanja wa golf wa Rais-mteule Donald Trump huko Bedminster. Ndege hizo pia hivi karibuni zilionekana katika maeneo ya pwani. Idara ya Upelelezi (FBI) ni kati ya mashirika kadhaa yanayofanya uchunguzi na wamewataka wakazi kutuma video, picha na taarifa nyingine walizonazo kuhusu droni hizo. - AP #newjersey #drones #us #voa