Wakazi kaunti ya Migori walalamikia uhalifu

  • | Citizen TV
    116 views

    Wakazi kaunti ya Migori, wameibua wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa visa vya uhalifu katika maeneo kadhaa ya Kaunti Ndogo ya Nyatike. Wakazi hao walisema wamerekodi visa vya mashambulizi na uvunjaji wa nyumba huko Sori na Macalder mtawalia. Katika kisa cha hivi punde, Mwanamme mwenye umri wa miaka 42 aliuawa, mkewe kujeruhiwa vibaya na binti yake wa miaka 14 kunajisiwa na majambazi kwenye shambulio katika ufuo wa Sori. Aidha wahalifu wamevunja ofisi kadhaa za serikali huko Macalder na mali kuibwa. Kamishna wa kaunti ya Migori Kisilu Mutua amesema polisi wanachunguza visa hivyo.