Wakazi wa Bomet wanataabika kupata maji

  • | Citizen TV
    497 views

    Wafanyabiashara na wakazi wa kaunti ya Bomet wanataka serikali ya kaunti hiyo iwajibike baada ya kukosa maji kwa miezi mitano sasa. Wamiliki wa hoteli wanasema kuwa biashara zao zimeathirika pakubwa kwa sababu wanalazimika kutumia maji chafu yenye gharama ya juu huku wakihatarisha afya ya wateja wao. Hata hivyo, wanasema kuwa wamekerwa zaidi baada ya gavana wa kaunti hiyo Hillary Barchok kuwaahidi kuwa usambazaji wa maji utaimarishwa ila wakazi wamesalia kwenye ngojangoja zisizo na mwisho.Inasemekana kuwa kaunti hiyo ina deni kubwa la kampuni ya usambazaji wa umeme