Wakazi wa cheptalal waandamana wakilalamikia huduma duni Bomet

  • | Citizen TV
    111 views

    Wakazi wa kijiji cha Cheptalal eneobunge la Konoin kaunti ya Bomet wameandamana kulalamikia visa vingi vya utepetevu wa matabibu katika kaunti hiyo. Kulingana nao, uzembe umesababisha vifo vya watu wengi kisa cha hivi maajuzi kikiwa cha mama mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliaga dunia baada ya kujifungua pale ambapo ambulensi ilikosa betri na mafuta ya kumhamisha hadi hospitali ya rufaa ya Longisa ili apate matibabu ya dharura.