Wakazi wa Gaza wakifurahia taarifa za mpango wa kusitisha mapigano

  • | BBC Swahili
    133 views
    Umati wa watu huko Gaza na Israel umeonesha furaha na hisia mseto baada ya kutangazwa mpango wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas katika mazungumzo yaliyofanyika mji mkuu wa Qatar, Doha. Mjini Washington, Rais Biden alisema awamu ya kwanza itawaruhusu Wapalestina kurejea nyumbani katika vitongoji vyao na kuruhusu misaada zaidi ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Umati wa watu ulishangilia huko Gaza, huku Israeli ndugu wa mateka wanaoshikiliwa na Hamas wakikumbatiana mitaani. #bbcswahili #Gaza #hamas Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw