Wakazi wa Oljorai, Nakuru waandamana kulalamikia unyakuzi wa ardhi yao

  • | KBC Video
    30 views

    Baadhi ya wakazi wa eneo la Oljorai katika kaunti ya Nakuru waliandamana kulalamikia kile walichotaja kuwa njama ya unyakuzi wa ardhi yao na watu mashuhuri serikalini. Wakazi hao waliojawa ghadhabu waliwakashifu vikali wale wamnaopanga njama hiyo wakiapa kuwa katu hawataondoka kwenye ardhi hiyo ambayo wanasema ni urithi walioachiwa na mababu zao. Wakiongozwa na aliyekuwa mwakilishi wadi wa eneo hilo John Ole Seina wakazi hao wanasema walikabidhiwa ardhi hiyo na hayati rais Daniel Moi na wanatoa wito Kwa serikali kuingilia kati na kusitisha mpango huo unaolenga kuhujumu haki yao ya kimsingi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive