Wakenya waendelea kutatizika na kulalamikia gharama ya juu ya usafiri

  • | Citizen TV
    1,052 views

    Jioni ya leo wakenya wameendelea kutatizika na kulalamikia gharama ya juu ya usafiri, kwenye mkesha wa sikukuu ya krismasi. Abiria wengi wakilalamikia kupanda maradufu kwa gharama ya nauli huku wengine wakiamua kutumia zaidi usafiri wa reli msimu huu wa sikukuu. Na kama Raphael Wangutusi anavyotuarifu, utafiti wa punde wa kampuni ya Infotrak pia unaashiria kuwa asilimia 60 ya wakenya wanasema krismasi ya mwaka imekuwa ngumu