Wakongo wakimbilia Burundi kupitia mto

  • | BBC Swahili
    2,794 views
    Zaidi ya watu 50,000 wamekimbia mashariki mwa DRC na kuelekea Burundi, wakihatarisha maisha yao kwa kuogelea katika mto Rusizi wakibeba na mali zao. Zaidi ya watu 20 wamefariki katika muda wa wiki mbili, na walionusurika wanadai walilikimbia jeshi la M23, ingawa BBC haiwezi kulithibitisha hili. Kutokana na hatua ya M23 kusonga mbele, hofu inaendelea kuwa Burundi inaweza kuwa si salama pia. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw