- 579 viewsDuration: 3:16Walimu na familia zao sasa wanatarajiwa kuhamia bima ya matibabu ya SHA baada ya mkataba wa bima ya kibinafsi wa shilingi bilioni 20 kukamilika. Tume ya kuwaajiri walimu (TSC) imetangaza kuwa uhamisho huo utaanza kutekelezwa tarehe mosi Disemba mwaka huu. Walimu wanatarajiwa kupata bima kamili kupitia mpango wa SHA, lakini wameonya kuwa iwapo mpango huo wa serikali hautatimiza matarajio yao, basi wataifutilia mbali bima hiyo.