- 440 viewsDuration: 1:16Chama cha walimu nchini KNUT tawi la Makueni kimepinga vikali mpango wa serikali wa kuwahamisha walimu kutoka bima ya matibabu ya kibinafsi na kuwaweka chini ya bima ya SHA. Katibu wa chama hicho kaunti ya Makueni Benson Ndambuki anasema hatua hiyo ni hujuma kwa walimu kwani wafanyikazi wengine wa umma wamewekwa chini ya bima za kibinafsi. Ameonya TSC kuwa huenda hatua hiyo ikalazimisha walimu kufanya mgomo wa kitaifa januari kuipinga.