Waliofariki kwenye mafuriko mai mahiu wafikia 60

  • | Citizen TV
    712 views

    Idadi ya watu waliofariki katika mkasa wa mafuriko Mai Mahiu imefikia watu sitini baada ya miili mingine miwili kuondolewa kwenye matope wiki moja tangu maporomoko kutokea. Kamishna wa kaunti ya Nakuru Loyford Kibaara amesema kuwa watu 23 kati ya 112 waliokuwa hospitalini wanaendelea kutibiwa huku shughuli ya kuwasaidia wakaazi walioathirika ikiendelea. watu 30 bado wanatafutwa huku maafisa wa kijeshi na wale wa Huduma kwa taifa -NYS- wakiendelea kushirikiana katika shughuli hiyo. Kibaara pia anasema kuwa juhudi zaidi zinafanywa ikiwemo kufuata mkondo wa maji ambao sasa umefikia kilomita sitini kuelekea katika kaunti jirani ya Narok. Ibada ya wafuu inatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi.